DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, December 27, 2013

Bibo: Khanga Pati 2014

 
Baada ya kufanya vyema kwa kuachia kichupa chake kipya kilicholeta mapinduzi makubwa katika swala la utayarishaji wake kilichobatizwa jina 'Ujuzi', msanii Climax Bibo ameiambia enewz kuwa anatarajia kuufungua mwaka mpya kwa kutoa kibao kipya cha 'Khanga Pati'.

Mkali huyo anayevuma sana kwa michano nchini amesema kuwa kazi nzima ya matayarisho ya trak hiyo inayofanyiwa kazi na prodyuza Benjamin Busungu inatarajiwa kukamilika kabla ya siku ya jumanne ya wiki ijayo.

Aidha Climax ambaye pia navutiwa kupiga kazi na baadhi ya wasanii wakali katika game amesema kuwa kuanzia mwakani ana mpango huo wa colabo hizo kwani mwaka huu Climax alitaka kuwaonyesha mashabiki wake kuwa ana uwezo

mkubwa wa kusimama yeye mwenyewe kupitia kazi zake saafi zikiwemo, Ghetto Boy, Ujuzi na sasa jiandaeni kwa Khanga Pati'

No comments: