DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Monday, December 23, 2013

Chege kutoa zawadi Xmas

 
Akiwa anajiandaa kutoa zawadi mpya kwa mashabiki wake katika kipindi hiki cha Krismasi msanii Chegge Chigunda ameelezea kuwa muda si mrefu anatarajia kuachia kichupa chake kipya kilichobatizwa jina 'Chapa nyingine' wimbo ambao unatarajiwa kuachiwa wiki hii jijini Dar es Salaam.

Meneja wa TMK, Said Fella amesema kuwa kichupa hicho kimeanza kufanyiwa kazi tangu wiki iliyopita ambapo ameelezea kuwa kama itafanyiwa uhariri mapema itakuwa ni zawadi tosha kwa mashabiki katika kipindi hiki cha shererhe za Krismasi.

Hadi hivi sasa wadau na mashabiki wanasubiri kuona kazi hiyo mpya inayofanyiwa kazi chini ya Director Adam Juma hivyo kaeni mkao wa kula wa kichupa hicho kipya kitakachoanza kusambazwa ndani ya wiki hii

No comments: