DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, December 27, 2013

Fella ajipnaga kuiteka 2014


 
Huku mwaka 2013 ukiwa unakaribia kabisa kumalizika msanii kinda wa muziki wa kizazi kipya nchini, Asilahi Isihaka ama 'Dogo Aslay' hivi sasa anatarajia kuachia wimbo wake mpya unaotarajia kutoka mwezi January mwakani unaokwenda kwa jina la 'Tulia'.

Kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Family anayemiliki pia kundi chipukizi la kituo cha Mkubwa na Wanawe kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam, ameiambia enewz kuwa hiyo ni moja ya ngoma mpya ambayo Dogo Aslay anaifanyia kazi, ambapo kwa sasa kichupa cha msanii huyo 'Ya Moto' kutoka kwao Mkubwa na wanawe kinaendelea kutikisa Afrika Mashariki.

Said Fella ambaye ameonyesha mafanikio makubwa katika kuinua vipaji na kulisimamia vyema kundi la TMK amesema kuwa mwaka 2014 utakuwa ni wenye mafanikio makubwa, kwani tayari kuna kazi mpya za wasanii kama Mh.Temba pamoja na Kassim Mganga ambao nao watatoa audio ya wimbo wao mpya mwezi January.

Aidha Fella amesema kuwa katika ngoma yake mpya Dogo Aslay ameweza kuwashirikisha wasanii wenzake wa kundi hilo la mkubwa fella na wanawe, huku akiwamwagia sifa wasanii hao chipukizi kwa kuweza kusimama vyema kwenye gemu.

No comments: