Kila mtu hupenda
kumalizia mwaka nyumbani, kama ilivyo kwa msanii huyu mahiri wa kizazi
kipya rapper Izzo Bizness … anatarajia kuwapa zawadi kubwa watu wake wa
nyumbani alipozaliwa na kukulia mwisho wa mwaka huu. Rapper huyu mkali
imeripotiwa kuwa siku ya tarehe 31/12/2013 kama wenzetu wazungu waitavyo
New Years Eve, basi rapper huyu atapiga bonge la shoo jijini Mbeya kwa
ajili ya kuuaga mwaka wa 2013 ambapo umekuwa mwaka mzuri kwa msanii huyu
katika industry ya music na kuukaribisha mwaka mpya wa 2014.
Shoo hiyo ambayo rapper huyu ataperform itakwenda kwa jina la Home
Sweet Home, litakalokuwa likifanyika katika Club ya Babz jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment