DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Monday, December 23, 2013

Jaguar amuunga mkono Sonko

 
Msanii wa muziki wa nchini Kenya Jaguar ameonyesha sapoti yake katika kampeni ya kupambana na silaha za moto nchini humo, kampeni ambazo zimeasisiwa na Seneta wa Jiji la Nairobi, Mike Sonko.

Msanii huyu atasaidia kutumia nafasi yake kama mtu mashuhuri, kuhamasisha wale wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha kwa vyombo vya dola ili kupambana na tatizo la uhalifu na kuimarisha usalama wa raia.

Katika kampeni hii, Seneta Mike Sonko ameahidi kitita cha pesa pamoja na ulinzi wa uhakika kwa yeyote yule atakayesalimisha silaha aliyonayo.

No comments: