DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, December 27, 2013

Jaguar Awasaidia Wafungwa Siku Ya Christmas …

ja 


Kama inavyokuwa wakati inapofikia msimu wa Christmas na mwaka mpya, kila mtu hupenda kusherekea siku kuu hizi na ndugu zao, marafiki au watu wakaribu. Lakini kuna baadhi ya watu hushindwa kusherekea siku hizi kutokana na kutokuwa huru (Wafungwa).
Msanii wa Kenya yeye aliamua kufanya kitu tofauti na wengine siku ya Christmas baada ya kuchukuwa uamuzi wa kwenda kuwatembelea wafungwa na kuwapatia zawadi kadhaa na pia kula nao chakula kama kuonyesha upendo kwa wafungwa hao ambao ni jambo ngumu kwao kusherekea siku kuu hiyo ya Christmas.

jag
 Msanii huyo pia alishinda mchana na usiku kucha na wafungwa hao katika Industrial Area prison huko nchini Kenya, na kuwasaidia wafungwa watano wenye makosa madogo kwa kuwatolea dhamana, ili waweze kuona familia zao msimu huu wa Christmas.

No comments: