
Mtoto Moureen Julius(12), amejinyakulia kitita cha shilingi Milioni tano katika fainali za Shindano la “MO KIDS GOT TALENT
2013” lililofanyika kwenye hoteli ya Ledger Plaza Bahari beach
lililoanza tarehe 25 hadi tarehe 28 mwezi huu ambapo fainali
zilifanyika.
Shindano hilo lilijumuisha watoto zaidi ya mia mbili ambapo kila mmoja alijipatia nafasi ya kuonesha kipaji chake vikiwemo kuogelea, kuimba, kucheza, karate na vingine vingi.
Watoto 15 walichuana katika nusu fainali na kuchujwa hadi kufikia
watoto watano na mwisho wa siku kupatikana SUPA STAA Moureen Julius
aliyewafunika wenzake kwa kipaji alichonacho.
Akizungumza na waandishi wa habari mara
baada ya kutangazwa mshindi wa kwanza aliyejinyakulia kitita cha
sh.millioni tano, Mtoto Moureen Julius alisema pesa hizo alizoshinda
atazitumia kwa kulipia ada na vifaa vingine vya shule.
Shindano hili la “MO KIDS GOT TALENT 2013″ liliandaliwa na Frost
Africa na kudhaminiwa na Mohammed Enterprises Tanzania Ltd. (MeTL)
Group.
ijana Salum Nyangumwe (17)
mshindi wa pili aliyeimba wimbo wa My Number One wa Msanii Nasib Abdul
a.k.a Diamond wakati wa fainali za kusaka kipaji cha SUPA STAA wa watoto
na vijana! la ”MO Kids Got Talent 2013″ lililofanyika mwishoni mwa Juma
kwenye Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini washiriki
wa shindano la “MO Kids Got Talent 2013″ wakiendelea kuonyesha vipaji
vyao wakati wa fainali za shindano hilo.

Pichani juu na chini washiriki
wa shindano la “MO Kids Got Talent 2013″ wakiendelea kuonyesha vipaji
vyao wakati wa fainali za shindano hilo.
Jaji Hidaya Njaidi akitoa
maoni yake kwa washiriki (hawapo pichani) waliokuwa wakichuana kuwani
Shilingi Milioni 5 za Kitanzania zilizotolewa zawadi na Kampuni ya MeTL
Group.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Frost Africa, Bw. Peter Sekasiko ambao ndio waandaji wa mashindano hayo na Meneja
Masoko Msaidizi wa MeTL Group, Bw. Aunali Bandali (kulia) wakifuatilia
kwa umakini mashindano hayo yaliyomalizika mwishoni mwa Juma.
Jaji Mkuu wa shindano la “MO Kids Got Talent 2013″ Salma Mziray akitoa maoni yake kwa washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora.
kwa habari zaidi bonyeza hapa
No comments:
Post a Comment