Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, D'Banj amesema kuwa atashirikiana
pamoja na Shirika Kimataifa la ONE katika mpango wake wa kueleza umuhimu
wa Kilimo kwa Vijana ili kuwasaidia kujikwamua na umasikini.
D'Banj ambaye amekutana na wadau kutoka shirika hili la ONE huko Afrika Kusini, amesema ameweza kufahamu manufaa makubwa ya kilimo, na atajitahidi kutumia umaarufu wake kufikia vijana wengi zaidi kuwaeleza juu ya kilimo, huku yeye mwenyewe akionyesha mfano kwa kuwa na mashamba yake.
Kwa mujibu wa D'Banj, baada ya kuzungumza na waratibu wa kampeni hizi za ONE, amegundua kuwa Kilimo ndiyo njia kuu ya kuikomboa Nigeria na Afrika kwa ujumla kutoka janga la umasikini.

No comments:
Post a Comment