DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, January 29, 2014

Lamar kuja na show ya TV

 
 Prodyuza mkali kabisa wa muziki hapa Bongo, Lamar ameweka wazi mipango yake ya kuanzisha kipindi chake cha televisheni cha uhalisia ambacho kitakuwa kinaonyesha maisha yake hususan katika kazi zake za muziki.

Lamar amesema kuwa, kipindi hiki kina lengo la kuonyesha ni jinsi gani anavyofanya kazi zake na pia namna anavyoshirikiana na wasanii wakubwa kutengeneza hits.

Lamar amesema kuwa, kipindi chake kitaanza hivi karibuni na kitakuwa tofauti sana na vipindi vingine kutokana na kuwa na lengo kuonyesha wapenzi wa muziki mchakato mzima wa kutengeneza muziki mzuri unavyokwenda.

No comments: