DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, January 29, 2014

Nameless kutoka na B4IR

 

 Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Nameless amewataka mashabiki wake kukaa tayari kwa video ya kazi yake mpya inayokwenda kwa jina B4IR, video ambayo itakuwa ni ya kwanza kabisa kutoka kwake tangu kuanza kwa mwaka 2014.

Hii ni moja kati ya mikakati ya msanii huyu mahiri kurudi katika game ya muziki baada ya kimya kirefu akiwa anaandaa kazi mpya pamoja na kutunza familia yake.

Nameless pia amewataka mashabiki wake kujua kua mzigo kamili.. Albam yenye nyimbo 20 ipo tayari kwaajili yao, na hadi kufikia mwezi Machi atakuwa ameshaiachia.

No comments: