Kwa hisani ya TFCA
Mahojiano
haya yametokana na -C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 98.
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya
Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:- ii. Mheshimiwa Spika,
kumekuwa na kilio cha muda mrefu cha wasanii kudurufiwa kazi zao za
sanaa na kukosa maslahi kwa kazi wanazofanya.
Ili
kutatua tatizo hili, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza
kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa nia ya
kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na hivyo kuzuia vitendo vya
kudurufu kazi za sanaa (piracy of artists work) hali ambayo inadumaza
ukuaji wa sanaa na vipaji hapa nchini.
Aidha,
Mamlaka ya Mapato itaweka stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi
hizo uwe rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili kutokana na
kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikali mapato. 80 Kwa kuwa
yanahitajika maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kurekebisha sheria
na kanuni mbalimbali, utekelezaji wa hatua hii umeanza rasmi tarehe 1
Januari, 2013.
Tunaangalia
uelewa wa wadau kuhusiana na hili na nini kifanyike ili kuweza
kuboresha sheria husiaka ili iendane na taratibu na miongozo itakayoweza
kuleta ukombozi wa kweli.
No comments:
Post a Comment