DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, August 30, 2013

DIAMOND PLATNUMZ AMEMZAWADIA MZEE NGURUMO GARI



Msanii wa kizazi kipya Naseeb Abdul aka Diamond Platinum baada ya kuzindua video ya wimbo wake mpya Number One au Namba 1 katika hotel ya kifahari Serena iliyopo jijini Dar es Salaam ambapo walihudhuria wadau mbalimbali wa hapa nchini.
Katika uzinduzi huo wa video ya wimbo wake mpya Number One Diamond alichukua fursa na kuamua kuongea machache kuhusu kustaafu kwa msanii Mkongwe ‘Ngurumo’ na kutoa heshima zake za dhati kwa msanii huyo mkongwe.




Diamond alisema amesikitshwa sana baada ya kusikia katika vyombo vya habari kwamba Ngurumo toka enzi za ujana wake hajawahi kumiliki gari,na hapo ndipo aliamua kuchukua nafasi na kumpa zawadi Ngurumo gari aina ya Funcargo.
Diamond Platnumz pia aliweza kutoa shukrani zake kwa watu wote waliofika kwenye uzinduzi huo wa video ya my number one.

No comments: