DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!
RAY C! MUNGU ANATAKA KUKUTUMIA!
Mungu
ametumia mkono wa wahalifu kukuteua, na akatumia mkono wa Mhe. Rais
Kikwete kuidhinisha uteuzi wake na sasa taifa linasubiri utendaji kazi.
Ni kwa njia yako wengi watapona maana vita hii ni ngumu sana kupigwa kwa
mtutu wa bunduki na makucha ya Serikali kama ambavyo watu wengi
wanadhani. Kwani Serikali zenye nguvu kubwa za kisayansi, kijasusi na
kijeshi na sheria ngumu ngumu kama vile Marekani, China, Uingereza nk
zenyewe zimeshindwa.
Ushauri
wangu mkuu kwako Mpendwa Ray C. Ni wakati Muafaka sasa kwako kuanzisha
asasi (NGO) kubwa isiyo ya kiserikali kwa ajili ya kupambana na madawa
ya kulevya, asasi ambayo uwe na majukumua makubwa matatu (1) Kuhakikisha
waathirika wanapata matibabu na kuacha madawa ya kulevya (2) kutoa
Elimu kubwa kwa jamii kupitia vyombo vya
habari, mashuleni na vyuoni na katika vikundi vya michezo nk (3)
Kupambana na wauza madawa ya kulevya Kisaikolojia kwa kuendesha kampeni
ya Elimu ya Kifikra itakayowashawishi kuacha wenyewe biashara hiyo.
Kwa
kupitia asasi (NGO) hiyo namshauri Rais Dr. Jakaya Kikwete aoneshe
Huruma na Uzazi kwa vijana na Watanzania wote kama alivyofanya kwa Ray C
kwa kusaidia NGO kupata uwezo wa kutekeleza majukumu yake. Ni matumaini
yangu kwa msukumo wa Rais Kikwete na umuhimu wake Asasi hiyo itapata
wafadhili wakubwa na kufanikisha malengo yake, kama alivyofanikisha
ufadhili katika Timu ya Taifa na mambo mengine kadha wa kadha..
No comments:
Post a Comment