DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Monday, September 30, 2013

DARASA: BADO WATU HAWAJAUELEWA MZIKI WANGU




 

Darasa ni mmoja kati ya wasanii wachache wa Hip Hop Bongo wenye uwezo mkubwa wa kuandika mistari yenye conscious za kutosha ndani yake huku ikiigusa jamii moja kwa moja. Lakini mbali na kujitahidi kuikomboa jamii kwenye mambo mbalimbali huku elimu ikihusika kikamilifu ndani ya tungo zake, Darasa anasikitishwa na watu kutomuelewa juu ya kile anachokiimba.

“Uandishi wa ngoma zangu huwa unanigharimu muda mwingi sana kufikiri na hata nguvu nyingi pia, lakini kinachonisikitisha wadau na fans wa mziki wa Bongo fleva hapa Bongo bado hawajauelewa mziki wangu na hata baadhi ya wanaonielewa hunielewa vingine pia.” – Darasa amefunguka. Mziki wa Hip Hop unahitaji uwezo mkubwa wa kufikiri na utulivu wa hali ya juu ili kuelewa nini kinachoongelewa ndani ya ngoma hiyo kutokana na artists wengi wa real hip hop, kutumia lugha ya picha na lugha ngumu kidogo isiyoeleweka haraka.

No comments: