
Msanii wa muziki ambaye anafanya kazi zake chini ya lebo ya B Hitz, Deddy ambaye style yake ya muziki anayofanya, Dancehall ndiyo imemfanya kutambulika vizuri katika gemu hapa Bongo, ameongea na eNewz kuhusiana na ni kwanini amekuwa akifanyakazi zake kwa machale sana, tofauti na wasanii wengine ambao kila baada ya kipindi kifupi huwa wanatoa kazi mpya.
Deddy ambaye kama ulikuwa hufahamu, ni mtoto wa mwanamuziki mkongwe Juma Kakere, amesema kuwa kuna kazi kibao ambazo amekua akizifanya na kuziweka, na kutokana na kuwa anafanyakazi chini ya menejiment, kuna mpango maalum ambao tayari umewekwa kwa ajili ya kuziachia.
Deddy amewataka mashabiki wake kukaa tayari kwasababu mipango ya yeye kuingia ka kasi katika soko la muziki bongo na mawe yake mwenyewe imeshasukwa vizuri na hivi karibuni ataanza kuachia mawe kwa mpangilio ambao tayari umeshasukwa vizuri.
No comments:
Post a Comment