Hizi ni
baadhi ya picha zikionesha jinsi ambavyo Tamasha la #KiliMusicTour2013
lilivyotikisa jiji la Dar-es-salaam. Umati mkubwa wa watu na wasanii
walifanya kazi kubwa sana kwenye stage. Wasanii waliopanda jukwaani
kuwakilisha #KikwetuKwetu ni: Mashujaa Band, Mzee Yusuph, Ras Six,
Recho, Linex, Ben Pol, Ney wa Mitego, Madee, Kala Jeremiah, ROMA, Joh
Makini, Lady Jay Dee, Profesa Jay na Diamond Platnumz. — in Dar es Salaam, Tanzania.

Siwasikiiiii.... Ndivyo Diamond Platnumz alivyowauliza wakazi wa Dar, nao kwa pamoja na mtikisiko mkubwa wakapiga kelele ambazo hazijawahi kutokea. — in Dar es Salaam, Tanzania.

Zawadi kutoka Kilimanjaro Premium Lager ziliendelea kutolewa na ma-MC wa usiku huu, Dullah na Zembwela.

Anaconda Lady Jay Dee alifanya surprize ya aina yake kwa kugonga remix ya Joto/Hasira aliyowashirikisha Moko wa Miujiza 'One The Incredible', Baba Malcom Nikki Mbishi na Profesa Jize!

Zawadi kutoka Kilimanjaro Premium Lager ziliendelea kutolewa na ma-MC wa usiku huu, Dullah na Zembwela.

Dansa wa Mzee Yusuph akionesha umahiri wa kukicheza kiduku.


Ras Six msanii wa reggae naye alikinukisha ile mbaya!

DJ AD Mafuvu aliwarusha mashabiki mwanzo mwisho!

Mwanadada Recho naye alifanya yake stejini.

Mkali wa masauti Ben Pol hapa akiimba wimbo wake mpya wa Ubani aliyomshirikisha mwanadada Alice.

Rais wa Manzese, Madee alipokelewa kwa staili yake na mashabiki.

Mwamba wa Kaskazini Mweusi Joh Makini naye alionesha zile zake ngumu nyeusi!

Kala Jeremiah aliwarusha mashabiki mpaka wakasema 'rahaaa'
No comments:
Post a Comment