
Wasanii wa Uganda, Peter Miles pamoja na Cindy Sanyu ambao wamekuwa nchini Kenya katika kipindi hiki cha shambulio la kigaidi, wameguswa kila mmoja kwa nafasi yake na tukio hili la kinyama kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.
Peter pamoja na Cindy kila mmoja kwa nafasi yake, wamechukua hatua mbalimbali ikiwepo ile ya Cindy kufanya onyesho lake kuwa maalum kwa waathirika wote wa shambulio hili.
Mpaka sasa bado jitihada zinaendelea kudhibiti eneo la kibiashara la Westgate huko Nairobi, ambalo bado ndani yake kuna magaidi wa al-Shabab wanaodaiwa kuwa ndio wanahusika na shambulizi hili.
No comments:
Post a Comment