Usaili kuanza kesho:
Tusker
Project Fame, shoo halisi ya muziki ambayo inapagawisha watazamaji na mashabiki
kwa ujumla Mashariki mwa Afrika. Sasa imerudi tena katika msimu wa 6 ambapo
msimu huu itakua ya aina yake kwa ukubwa na nzuri zaidi kulinganisha na misimu
iliyopita.
Miliki
jukwaa! Tusker inawaalika wale wote wenye vipaji vya kuimba kufika katika
usaili tarehe 7 na 8 Septemba, 2013 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini
Dar es Salaam. Baada ya hapo washiriki wa Tanzania watapata nafasi ya kuingia
katika jumba la Tusker project Fame na kushindanishwa jukwaani na vinara kutoka
Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini.
Zawadi
ni nono msimu huu, na mshindi wa Tusker project Fame atajinyakulia kitita cha Sh.
100,000,000 za kitanzania na kupata mkataba mnono wa mwaka wa kurekodi wenye thamani ya Sh. 200,000,000 za
kitanzania. Ni imani yetu kwamba fedha zitabebwa na mtanzania kwani vipaji
tunavyo vya kutosha kikubwa watanzania wajitokeze kwa wingi katika usaili huu.
Katika
msimu huu mpya watu wengi zaidi watahusika katika shughuli mbalimbali uwanjani
hata kumiliki jukwaa. Kujiunga na hayo yote shiriki katika promosheni
zinazoendelea katika bar mbalimbali na upate ofa za Tusker.
KUHUSU USAILI
Tusker Project Fame kupitia bia yake ya
Tusker Lager inatafuta vijana wenye vipaji vya kuimba nawenye uwezo wa kuleta
mabadiliko katika soko la muziki pia wenye utaalamu wa hali ya juu katika
kuimba na kutumia vifaa vya muziki ipasavyo. Wapenzi wote wa muziki ambao wana
weledi wa kutosha kuiwakilisha Tanzania na kuonesha kuwa wanaweza kufanikiwa na
kujulikana kama nyota katika muziki wanakaribishwa sana.
Wale
wenye vipaji vya muziki wanaweza kujaribu bahati kwa kujitokeza katika usahili
wa Tusker project fame. Siku mbili za usaili kwa ajili ya kusaka mastaa wa msimu
wa 6 wa Tusker Project fame utakaofanyika jijini Dar es Salaam kama ifuatavyo:
Tarehe
7 Septemba 2013, Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili
asubuhi
Tarehe
8 Septemba 2013, Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa mbili
asubuhi
Washiriki
waje wakiwa tayari kuwakabili majaji wetu ambao wataangalia kipaji, kujiamini
na kubwa zaidi wataangalia washiriki ambao wateweza kufundishika na wale
watakaoibuka vinara kwa wenzie.
Usahili
wa Tusker Project Fame ni kwa wale wenye umri zaidi ya miaka 18.
ITAONYESHWA
Msimu
wa sita wa Tusker Project Fame inarushwa hewani kupitia katika vituo vya televisheni
vya EATV saa 2 usiku na ITV saa 4 usiku.

No comments:
Post a Comment