DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, September 27, 2013

Prezzo ateta na wasomi


 

CMB Prezzo kutoka Kenya, ameonyesha manufaa ya nafasi yake kama kioo cha jamii kwa kukutana na kuongea na wanafunzi wa chuo kikuu cha Daystar huko Nairobi na kubadilishana nao uzoefu kuhusiana na maswala muhimu yanayowahusu.

Prezzo ameonyesha furaha na kujivunia fursa hii kubwa ya kuzungumza na wasomi ambao nao pia wamepata fursa ya kujifunza mengi kutoka kwa msanii huyu wa muziki na pia mjasiriamali mwenye mafanikio katika jamii.

Nafasi hii ya Prezzo, imemkutanisha na wanafunzi wanaosoma dini ya Kikristo pamoja na maswala ya Media, Kitu ambacho pia kinatafsiriwa kama moja ya hatua ya msanii huyu kujirudisha karibu na Mungu wake.

No comments: