Menina akifanya yake
Vanessa
jukwaani akiimba Closer
Snura
Majanga akitoa burudani
Walter Chillambo akiimba
Mashabiki waliojitokeza
wakishangilia
Fuse ODG akifundishwa kucheza kiduku na shabiki
Wasanii wa Marco Chali Foundation
wakiwa katika picha ya pamoja.
======== =========== =========
MSANII wa muziki wa kileo kutoka nchini Ghana Fuse ODG, Azonto amezikonga
nyoyo za wapenzi wa burudani baada ya kuchanganya staili yake ya uchezaji Azonto
pamoja na ile ya Kiduku ya hapa nchini.
Fuse
ODG ambae anajulikana zaidi kama Azonto alipanda jukwanii majira ya saa tisa
kasoro usiku baada ya wasanii wengine wengi kumaliza kutoa burudani. Ilikuwa
ni baada ya kupanda kwa kundi la Tip Top Connection huku likiongozwa na msanii
Madee pamoja na msanii Chid Benz ambae aliimba nao kama msanii rafiki.
Baada
ya kumalizika kwa shoo hiyo kwa wasanii hao wa hapa nyumbani ndipo alipopanda
msanii Azonto ambae alisikika akihamaisha kwa kutajan maneno ya kiswahili kama
vile, Nawapenda, Mambo vip na piga kelele.
Msanii
huyo kwa kiasi kikubwa alifanikiwa kuwaweka karibu zaidi wapenzi wake wa
burudani hasa pale alipowapandisha jukwaani vijana wawili kucheza nao Azonto na
Kiduku.
Alianza
kwa kuwachezesha Azonto na kisha muda huo huo aliwabadilishia muziki na kucheza
nao kiduku huku mwenyewe akiahidi kuiendeleza zaidi staili hiyo.
Akizungumza
baada ya onesho hilo alisema kuwa amefurahishwa na namna ambavyo wasanii na
watu wa Dar es salaam walivyompokea na kuahidi kuwa ataiendeleza staili ya
kiduku nakuitangaza zaidi.
"Mimi
kwanza niliwahi kuja Tanzania na kufikia kule Arusha kwa mapumziko na kwa sasa
nimekuja kwa kazi na nipo tayari kufanya kazi na wasanii wa Tanzania kwani
mwisho wa siku sisi ni waafrika ambao tunatakiwa kusaidiana na
kuendelezana" alisema Azonto.
Wasanii
kama vile Madee, Tunda Man, Water Chilambo, Menina Atik, kundi la Navy Kenzo, B
Heats, Mabeste, Eskide, Mapacha na wengineo wengi pia walitoa burudani safi
siku hiyo.




No comments:
Post a Comment