Ikiwa imepita wiki zipatazo nane tangu amekuwa Baba, Rapa Mabeste ambaye anafanya kazi zake chini ya lebo ya B Hitz, ameelezea uzoefu wake kama baba wa familia, na kukiri kuwa ni maisha mapya ambayo yamembadilisha na kumfanya kuwa mtu mpya.
Kupitia mahojiano ambayo amefanya na eNewz, mabeste amesema kuwa sasahivi ameongeza bidii nyingi katika kufanya kzai kuhakikisha kuwa anasimamia majukumu yake yote ya kifamilia kikamilifu kama baba.
Kwa upande wa muziki wake pia, Mabeste amethibitisha ukomavu wake, ambapo amezungumzia ngoma yake inayokwenda kwa jina “Nishauri” ambayo amefanya na Peter Msechu ikiwa ni kama kazi inayolenga kuomba ushauri wa kile kinachofaa kufanya kama mtu mzima na mwenya majukumu katika jamii.
No comments:
Post a Comment