DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Sunday, September 1, 2013

WAKAZI WA MTWARA WALIPOKEA KWA KISHINDO TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 MWISHONI MWA WIKI.

Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Baba Levo akiwaimbisha wakazi wa Mtwara wimbo wake uitwao Polisi,kwenye tamasha la tamasha la Serengeti Fiesta 2013,lililofanyika kmwisho mwa wikend ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara
Ni shangwe za kutosha ndani uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Msanii wa Muziki wa bongofleva katika miondoko ya hip hop,aitwaye Godzilla akishusha mistari yake live kwa mashabiki wake ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona,mkoani Mtwara 
 Umati wa wakazi wa Mtwara ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013 usiku huu
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz akiwaimbisha wimbo wake wa Tupogo wakazi wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la serengeti fiesta  mwishoni mwa wiki ,mkoani Mtwara.
Mmoja wa wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Baba Levo akiwaimbisha wakazi wa Mtwara wimbo wake uitwao Polisi,mwishoni mwa wiki ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013. 
Msanii aliyeibuka kwa kasi hivi sasa katika muziki wa Bongofleva,aitwaye Snura akionesha staili ya Kuvurugwa jukwaani.
Baadhi ya Wakazi wa mkoa wa Mtwara na vitongozji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona mwishoni mwa wiki.
Anaitwa Dj Mully B akionesha umahiri wake wa kukamua mangoma mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 .
Mashabiki wa tamasha la burudani la Serengeti Fiesta 2013 wakifuatilia kwa makini yanayojiri kwenye tamasha hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara,ambapo wakazi wa mkoa huu kwa mara ya kwanza walishuhudia live tamasha hili ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
Wakishangweka safi kabisa usiku huu.
Ni burudani ya kutosha kabisa usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta ambapo maelfu ya watu wamejitokeza kuburudika ndani ya uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.
Snura na densas wake wakitumbuiza jukwaani 
Anaitwa Linah kutoka nyumba ya vipaji ya THT,akiimba jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa Mtwara waliojitokeza mwishoni mwa wiki kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Kijana mdogo,lakini anakuja kwa kasi kabisa katika anga ya muziki wa kizazi kipya,hasa hip hop,aitwaye kwa jina la kisanii Young Killer kutoka jijini Mwanza,akitumbuiza usiku huu mkoani Mtwara kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013.

No comments: