DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, October 3, 2013

D'Banj, Bebe Cool jukwaani Zimbabwe

 

Wasanii wakubwa Africa, D Banj kutoka Nijeria pamoja na Bebe Cool kutoka Uganda wanatarajia kuifanya tarehe 26 mwezi huu kuwa ni siku ya kihistoria kwa upande wa Burudani nchini Zimbabwe ambapo watakuwa wakifanya onyesho juu ya jukwaa moja.

Kivutio kikubwa zaidi kutoka katika onyesho linalotarajiwa kutoka kwa wasanii hawa ni taarifa kuwa kila mmoja wao atapanda jukwaani na bendi yake kutumbuiza, katika tamasha hili kubwa kabisa lililopatiwa jina  'The Battle of Africa'.

Wasanii wengine ambao wanatarajiwa kutengeneza vichwa vya habari kutoka katika onyesho hili kubwa ni pamoja na Wallace Chirumiko aka Winky D, King Shaddy pamoja na Guspy Warrior.

No comments: