
Bob Junior ametaja wivu kama moja ya sababu zilizofanya ndoa yake kuvunjika na kwamba alikuwa na wakati mgumu sana kumuonyesha mke wake kuwa yeye ni muaminifu kutokana na kuwa star na kupendwa na mashabiki wengi wa Kike.
Wakati huo huo kwa upande mwingine, Bob Junior pia kwa sasa ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina “Bashasha” akiwa amemshirikisha msanii wa kike anayekuja juu Vanessa Mdee, amewataka mashabiki kuipokea vizuri kazi hii mpya ambayo ina ujumbe mzito wa kimapenzi.
No comments:
Post a Comment