Msanii mahiri wa miondoko
ya rap nchini Tanzania AY, amefanikiwa kurudisha account yake ya
mtandao wa kijamii wa Twitter pamoja na E-mail yake baada ya wajanja wa
internet kufanikiwa kuingia katika akaunti zake hizo siku ya tarehe 20
November na kujaribu kuzitumia kutafuta masilahi yao.
Lakini msanii AY kupitia
msaada kutoka kwa manager wake wa Social Network, ambaye huwa anamanage
na kucontral akaunti za mtandao wa internet kwa ajili ya mawasiliano ya
msanii AY, alifanikiwa kuzirudisha account zake hizo kutoka kwa hacker
asiyejulikanika ambaye alibadilisha mpaka passwords za AY, lakini kwa
sasa akaunti hizo zisharudishwa mikononi mwa AY.
No comments:
Post a Comment