
Kus Ma ambaye ni mtayarishaji muziki mzuri pia, licha ya umri wake mdogo, amewashangaza wengi waliokuwa hawafahamu kipaji chake hiki cha kupiga muziki live, na hii ni hasa kutokana na kuzoeleka kwa swala kuwa wasanii na wanamuziki wengi wa sasa wamebobea katika muziki wa kidijitali tu.
Kus pamoja na Tiri ambao mbali na kufanya muziki pia ni wapenzi, wameendelea kuendeleza harakati zao za muziki kwa karibu wakiwa pamoja kwa muda sasa, na hii ni baada memba wengine wa kundi la Camp Mulla kuonekana kuwa bize na shughuli zao za binafsi.
No comments:
Post a Comment