
Mabeste Venance ndilo jina lililopo kwenye cheti chake cha kuzaliwa lakini anajulikana sana kama Mabeste ambaye ameshagonga hits nyingi kama Baadae sana, Dole n.k.
Mabeste amekuwa ni mmoja kati ya wasanii ambao wanaendelea siku baada ya siku kimaisha ya kawaida na mziki pia. Mbele ya BK cop alifunguka sababu ya kuwa tofauti na wengine kimaisha yake ya kila siku.
“Kila unachokiona kwangu kimetokana na mziki wangu maana ni mziki pekee ndo umenikutanisha na watu wengi ambao wamekuwa wakinishauri mambo mazuri na hata kuongeza connections.” – Mabeste.
“Lakini pia nimeweza kkuwa na mji wangu huku nikiimudu vyema familia yangu kwa sababu tu heshima nimeiweka mbele kwenye kazi yangu na yeyote anayehusika na kazi yangu kinamna yoyote.” – Mabeste.
Mabeste amebahatika kupata mtoto miezi miwili iliyopita na amepanga mengi sana ya kumfanyia mtoto wake huyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha anapata malezi bora ya baba na mama.
No comments:
Post a Comment