
Kwa sasa Chismo ameshasaini mkataba huo na yupo mbioni kukamilisha video yake ya kwanza na pia ameshaanza kurecord nyimbo katika studio tofauti tofauti za hapa nchini akiwa chini ya kampuni hiyo.

Kwa upande wake Chismo amfunguka na kusema “nilianza mziki kama dansa na nilifanya kazi ya udansa kwa Bob Junior nikatoka nikaenda kwa Dully Sykes na ndipo nikaamua kuungana na Baby J lakini ndoto yangu haikukamilika na kuna kipindi nilimuomba msaada Tunda Man na akanikubalia kwakua alikua anaona uwezo wangu ila muda ulivyo zidi kwenda ndio nikakutana na Rich Mavoco na nikafanya nae pia kazi lakini nikiwa nae mazoezini, nilikua naimba nyimbo yangu ya Folow me na yeye alikua anaipenda sana na akawa ananirekodi kumbe, mwezangu akaingia studio na kufanya kweli, Kote nilipopita huko ilikuwa kama sehemu yangu ya kujifunzia tu.
No comments:
Post a Comment