
UKIONGELEA asilimia kubwa ya filmu kubwa na nyingi Swahiliwood ukiuliza nani kaandika basi utaambiwa ni mwandishi mahiri wa mswada Bongo ni Ali Yakuti, halina ubishi yeye ndio mwandishi anayetesa hivi sasa kwa kuwa na filamu nyingi zilizoandikwa na yeye, lakini ukiongelea waandishi wanaokuja kwa kasi basi jina la Said Mkukila naye anayesikika kufuata nyayo za Yakuti.

“Kuna watu wananifananisha na waandishi wakubwa waliofanikiwa katika tasnia ya filamu lakini mimi sijifananishi na mtu mwingine kwani kila mtu ana wakati wake na hata mfumo wa uandishi pia unaweza kutofautina kulingana na mapokeo ya stori yenyewe,”anasema Mkukila.
Mwandishi huyo ambaye anaonyesha uchu wa kujifunza na kuwa mwandishi wa kimataifa siku zijazo na kuwa mkombozi wa tasnia ya filamu Bongo, Mkukila hadi sasa amendikia script filamu kama Mbegu, Kigodoro akishirikiana na Omary Clayton, Machozi na Wazanga yangu ambazo zinafanya vizuri sokoni.
No comments:
Post a Comment