
Seneta amesema kuwa baada ya round kadhaa nje ya muziki, mashabiki wa muziki wake watarajie pini mpya kutoka kwake, pini ambayo imesukwa na prodyuza Tuddy Thomas, na ndani yake kukiwa na backup ya rapa Godzilla.
Kama ulikuwa hufahamu, eNewz tumekutana na msanii huyu katika mishe za kujipatia tiketi kadhaa za show ya P Square kwaajili yake na washkaji zake Jumamosi hii, Tukamuuliza anauzungumziaje ujio wa wasanii hawa, na mshkaji akaweka bayana kuwa hakuna sababu yoyote ya mpenda burudani kukosa kuhudhuria onyesho hili kubwa hasa kutokana na uwezo mkubwa wa wasanii hawa jukwaani pamoja na namna walivyoiteka tasnia ya Burudani kimataifa.
No comments:
Post a Comment