DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Wednesday, November 27, 2013

Shilole 'kijasho' kikaangoni

 

Baada ya kukukutanisha na mastaa mbalimbali na kukupatia nafasi kuchat nao live, Kikaangoni Live ya facebook EATV leo imekuletea burudani nyingine,  Shilole Kiuno live mtandaoni.

Kwa muda wa saa 2 nzima, Shilole ameweza kukaangwa na maswali ya mashabiki wake mwenyewe, kuhusiana na mambo mengi ambayo ni gumzo juu yake kuhusiana na shughuli zake za muziki, shows pamoja na maisha yake kwa ujumla.

eNewz tumefuatilia zoezi hili kwa karibu na mwishoni tukamwuliza Shilole kuhusiana na joto ya kikaango ambapo amekiri kuwa japokuwa kumekuwa na maswali magumu kutoka kwa mashabiki wake, ameweza kuyajibu vizuri na anafurahi kuchat na mashabiki wake.

Utaratibu ni kama hivi, Kila wiki tunakupatia nafasi ya kuchat na staa ama mtu maarufu umpendae ili uweze kusikia kile ambacho ulikuwa unataka kukifahamu kumhusu moja kwa moja kutoka kwake, endelea kushare ukurasa huu na marafiki, like kama bado hujafanya hivyo kwa ajili ya kuwa sehemu ya familia hii yenye maujanja kibao.
Unaweza kufuatilia zoezi la mazungumzo ya Shilole na mashabiki wake mtandaoni mchana wa leo hapa

No comments: