DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, January 7, 2014

Grand Pa, Candy wapo poa

 
Mkuu wa lebo ya Grand Pa pamoja na Mkuu wa lebo ya Candy n Candy zote kutoka nchini Kenya, Refigah pamoja na Joe Kairuki, kwa pamoja wameamua kuuthibitishia umma kuwa hakuna tofauti ya maelewano kati yao kama ambavyo imekuwa ikitafsiriwa na wengi.

Wakubwa hawa wamesema haya walipokutana mara ya kwanza uso kwa uso hivi karibuni huko Mjini Mombasa katika sherehe za tuzo za Coast Music.

Joe na Refigah walipoulizwa juu ya hili kwa nyakati tofauti, kila mmoja alisema kuwa lengo lao kubwa ni kusapoti vipaji vya muziki tu na si kuleta ushindani na ugomvi usio na mantiki.

No comments: