Rapper Wakazi kuanza
kutimiza ahadi ya mashabiki wake, baada ya msanii huyu wa Rap hapa
nchini Tanzania kutoa ahadi kwa wapenzi wa music industry mwishoni mwa
mwaka jana kuwa wategemee kazi za Audio na Video za kutosha kuanzia
mwanzoni mwa mwaka huu wa 2014 kutoka kwake. Wakazi anatarajia kuachia
wimbo na video yake mpya ya wimbo uitwao Sumu Ya Panya (My City).
Msanii
huyu ameanza kufanya kazi mpya hivi karibuni ikiwamo video hiyo ya
wimbo wake mpya wa Sumu Ya Panya, ambapo tayari msanii huyu ameashaanza
kushoot video, huku audio ya wimbo huo ukiwa umeshamalizika, video ya
wimbo huu ikikamilika utatoka pamoja na audio yake. Jana jumatatu ndio
siku ambayo msanii huyu alianza rasmi kushoot video… Tazama hapa baadhi
ya picha za msanii huyu akiwa kazini anafanya video ya Sumu Ya Panya (My
City)
No comments:
Post a Comment