Baada ya ukimya wa muda mrefu sasa, wasanii Mgosi Mkoloni pamoja na Dr
John wameamua kuwarejeshea mashabiki wa muziki wa Bongofleva ambayo
walikuwa wameikosa kwa muda mrefu, kwa kujiunga tena kama Wagosi wa Kaya
na kuachia kazi mpya mbili kwa pamoja
Kazi
za wasanii hawa ni video mbili za ngoma inayokwenda kwa jina Bao na
nyingine ikiwa inakwenda kwa jina Gahawa ambazo zote zimeachiwa ndani ya
siku moja, zikiwa ni kazi safi za video zilizofanywa na muongoza video
mahiri Mecky Kaloka, audio zake zikiwa zimefanyika katika studios za
Tongwe Records.
Wagosi wa Kaya wamefanya kazi hii maalum kwa kuwaonyesha mashabiki
kuwa bado wanaiweza michano, na hii ni baada ya miaka mingi ya kila
mmoja wao kujikita katika shughuli zake binafsi.
Kupitia video ya 'Bao' ambayo, wasanii hawa wamejaribu kutumia usanii
wao kuzungusha maneno ili kufikisha ujumbe maalum unaowalenga wapenzi
walio katika mahusino, hususan wanandoa juu ya namna ya kudumisha
mahusiano yao.
No comments:
Post a Comment