DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, April 17, 2014

Buriani Maalim Muhidin Gurumo

 
Nguli wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Muhidin Maalim Gurumo amezikwa leo kijijini kwao Masaki wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Kabla ya msafara kuanza kuelekea Masaki kwa maziko, Gurumo aliagwa na mashabiki na wapenzi wa muziki wa dansi nyumbani kwake Mabibo External Jijini Dar es Salaam, wakiongozwa na Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Muhidin Gurumo alifariki dunia juzi Jumapili katika hospitali ya Muhimbili baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala Pema Peponi Amina.
 
 
 
 

No comments: