Wasanii wakali kutoka Kenya, Collo pamoja na Nyashinski ambao kwa pamoja walikuwa wakiunda kundi mahiri la rap la Kleptomaniax, wamepanga kuungana na kufanya ujio mwingine mkubwa katika game, ikiwa ni miaka kadhaa tokea walipotengana.
Collo katika mahoajiano aliyoyafanya hivi karibuni, amesema kuwa ni kweli yeye na Nyashinski wamekwishaanza kutengeneza rekodi ya pamoja ambayo itakamilika ndani ya wiki kadhaa, na kazi hii inatarajiwa kulirudisha kundi hili katika chati za muziki Afrika mashariki kwa kishindo.
Mpango wa kurejea kwa kundi hili ambalo pia linamhusisha rapa Roba, unangojewa kwa msisimko mkubwa hasa kutokana wasanii hawa kuacha kufanya kazi pamoja wakiwa katika chati za juu kabisa, na mashabiki wao wakiwa bado na kiu ya kuendelea kusikiliza kazi zao.
No comments:
Post a Comment