DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, April 17, 2014

HAMMER Q AJIONDOA KWENYE KUNDI LA OFFSIDE TRICK

hammer-q
 
Msanii wa muziki wa Taarab na Bongo Flava, Hammer Q amejiondoa kwenye kundi la muziki la Offside Trick baada ya kuona hanufaiki na chochote.
Hammer Q ameiambia BK kuwa kwa sasa atakuwa akifanya kazi zake mwenyewe.
“Kwasasa hivi nimeamua kujishughulisha na mishemishe zangu mwenyewe kwasababu nimejiunga Offside Trick muda kidogo kama miaka miwili,lakini kilichotokea pale ni uvivu katika issue za kazi, yaAni kwamba mkisharekodi watu wanakuwa wavivu kufuatilia mambo ya kazi,sasa ile kwa upande wangu naona kama inanirudisha nyuma,” alisema.
“Sasa nikaona kwasababu mimi nina uwezo wangu binafsi tukiacha masuala ya Offside Trick niamue kwanza kufanya kazi kwanza mwenyewe,hakuna ugomvi uliotokea kwasasabu mimi mwenyewe binafsi yangu mambo ya ugomvi huwaga siyapendi, lakini kilichotokea kwangu mimi ni maslahi ya kuendelea kukaa pale,kwasababu tunaweza tukapanga tufanye dili hili na hili tukajiandalia show halafu mwisho wa siku mshikaji akachomoa, sasa hizi ni lawama na tunaharibiana kwa wale waandaji wa show wenyewe. Ukiangalia vitu kama hivyo ni moja wapo vimenisababisha nianze kufanya kazi zangu. Tunaweza tukapata issu sehemu fulani tukaalikwa, mshikaji anakataa kwasababu yeye ana studio inaingiza, mimi sina studio nategemea muziki ndio kazi yangu,” alisema Hammer Q.
Hammer Q amesema yeye na AT aliyejitoa kwenye kundi hili muda mrefu uliopita wamerekodi wimbo uitwao ‘Siri’.
 
Kuna kazi nafanya mimi na AT nadhani next wiki itakuwa ipo tayari,” amesema msanii huyo. “Mimi ni mkubwa sana katika muziki ugomvi wowote ambao umetokea mimi siuangalii kwababu sisi wote tumetoka kumoja,hatuitaji kushadadia issue za ugomvi kama hizo. Sijataka kuangalia chanzo cha ugomvi mimi nimeangalia uwezo wa kazi, kwamba nikikaa mimi na AT tunaweza tukafanya kitu kimoja kizuri sana. Kwahiyo sijataka kuangalia issue za ugomvi nataka tuonyeshe uwezo wa kazi, mimi na AT kila mmoja anafanya kazi kivyake sema sasa hivi kuna kazi ambayo nimeamua nifanye na AT kwa kipindi hiki,hatuzungumzii kundi, kila mmoja anatambua uwezo wa mwenzake ndio maana akakubali kufanya kazi na mimi. Hata mimi naelewa yeye ana uwezo wake binafsi ndio maana mimi nikakubali kufanya kazi na yeye,kwahiyo tunafanya kazi kama watu wawili yaani mimi na yeye, lakini sio kundi.”

No comments: