WERAWERAAA! Baada ya kuishi kwa muda mrefu tangu alipotengana na
mumewe Khamis Bwela, Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga
Pepeta’, Asha Baraka ‘Iron Lady’ usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita
alifunga ndoa na mfanyabiashara maarufu Dar aitwaye Idd Baka Pandisha,
Ijumaa Wikienda lina mzigo kamili.
Mkurugenzi wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka ‘Iron Lady akifunga ndoa na mfanyabiashara maarufu Dar aitwaye Idd Baka Pandisha usiku wa kuamkia ijumaa iliyopita. Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu, tukio hilo la aina yake lilijiri maeneo ya Magomeni-Usalama, Dar, nyumbani kwa mkurugenzi huyo ambapo watu wachache ndiyo waliohudhuria huku mdogo wa bi harusi, mama yake Nasibu Abdul ‘Diamond’ Sanura Kasim a.k.a Sandra akiwa ndiye msimamizi wa shughuli nzima.

No comments:
Post a Comment