Wasanii wanaowania tuzo za muziki wa Injili za Groove za huko nchini Kenya kwa mwaka 2014, wametangazwa majina yao, ambapo katika orodha hii msanii Size 8 kati ya wengine ameweza kungara kwa kutokea katika vipengele vitatu muhimu.
Kwa mujibu wa orodha hii, Size 8 akikabiliwa na wasanii wakali katika upande wa muziki wa injili ambao ameanza kuufanya muda si mrefu, anatokea katika kipengele cha Msanii bora wa kike wa mwaka, Wimbo bora wa mwaka na video bora wa mwaka kupitia rekodi yake ya Mateke.
Katika tuzo hizi, wasanii wengine wakali pia kama Jimmy Gait, Rufftone na Daddy Owen pia wanaingia katika baadhi ya vipengele na kufanya msisimko mkubwa kuelekea kuwatambua washindi halisi pale tuzo hizi zitakapotolewa, tarehe 3 mwezi Juni.

No comments:
Post a Comment