Msanii wa muziki C Pwaa, ametangaza ujio wake mpya akiwa chini ya
usimamizi wa lebo mpya ya Brainstorm Music, akiwa na mpango mkubwa wa
kubadilisha namna biashara ya muziki inavyokwenda sasa ili kumfaidisha
kila msanii.
C
Pwaa ambaye alituahidi hapo awali kuanza kutikisa mwaka 2014 kwa rekodi
kali kuanzia mwezi huu, amesema kuwa akiwa na uongozi huu mpya, wakati
wa kufanya rekodi kila kitu kitakuwa kinakwenda kwa makubaliano tofauti
na mambo ambavyo yanakwenda katika industry hii kwa sasa.
C Pwaa amesema kuwa, hii ni hatua ya awali katika kuingiza biashara
ya muziki hapa Tanzania katika mfumo ambao hutumika katika nchi nyingi
ambazo zimeendelea ambazo amepata nafasi ya kuzitembelea.
No comments:
Post a Comment