Mkali wa miondoko ya Dancehall kutoka nchini Jamaica, Konshens kwa mara
ya pili katika historia anatarajia kutua Jijini Nairobi kutumbuiza
katika onyesho kubwa litakalofanyika tarehe 12 mwezi Aprili.
Ujio
wa msanii huyu ni moja ya matukio makubwa kabisa katika historia ya
burudani nchini Kenya, akiwa bado anafanya vizuri kabisa na ngoma kali
kama vile Bounce, Walk n Wine, Gal a Bubble na nyinginezo.
Kwa upande mwingine, staa mwingine mkali wa Kimataifa wa miondoko ya Reggae, Gramps Morgan naye ametangaza kuwa, yupo tayari kabisa kwa ajili ya kufanya ziara kubwa Afrika, ambapo miongoni mwa nchi anazotazamia kuzifikia kwa burudani, Kenya vilevile Tanzania zinatokea kwenye orodha.

No comments:
Post a Comment