DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, August 13, 2013

“COLOUR KWA FACE”-NONINI FT CHRISTINE APONDI









Siku chache zilizopita nilipokea taarifa kutoka kwa Msanii Nonini kutoka nchini Kenya kwamba ameachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Colour kwa Face kutoka katika album yake ya tatu aliyoipa jina The Godfather of Genge(ipo sokoni hivi sasa) akimshirikisha mwanadada Christine Apondi. Kwa bahati mbaya sikupata muda wa chapchap wa kuusikiliza wimbo huu mpaka hivi leo.Kwa kawaida huwa siweki wimbo mpya hapa mpaka niwe nimeshausikiliza na kuupitisha(kuna watoto wanaingia hapa,lazima tuzingatie maadili fulani) Baada ya kuusikiliza ilinibidi kusitisha vyote nilivyokuwa nafanya,kwenda ndani,kutoka nje na kuketi tena.Katika wimbo huu Nonini ambaye ni mwanaharakati wa kutetea watu wenye ulemavu wa ngozi(albino)anatuma ujumbe mpana sana kupitia wimbo huu.
Kama mtakumbuka,Taifa letu la Tanzania liliingiwa na kashfa ya kimataifa pale ulimwengu ulipogundua kwamba kuna binadamu fulani wenye roho za ajabu wanawageuza watu wenye ulemavu wa ngozi “deal”.Nonini anaongelea hilo pamoja na mambo mengine ya kubaguana.Anaasa kupendana.Mpende kaka yako,mpende jirani na mpende kila mtu.Kwanini kubaguana? Wimbo umetengenezwa na Musyoka kutoka Decimal Records.Usikilize…



 Unaweza kutizama picha za Nonini akiwa katika harakati zake za kupinga ukatili wowote dhidi ya albinos kwa kubonyeza link hii http://www.noninimusic.com/v2/national-albinism-day-may-4th/

No comments: