DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, August 13, 2013

KINA BUSHOKE…





Ukisema kwamba Tanzania hakuna “familia za wanamuziki” utakuwa unakosea kwani jibu ni kwamba zipo. Mojawapo miongoni mwa familia hizo ni ile ya kina Bushoke. Pichani ni mwanamuziki ambaye hujulikana kwa jina la Bushoke ambaye ni mtoto wa Max Bushoke, mwanamuziki mkongwe wa Tanzania ambaye siku hizi anafanya kazi ya utangazaji nchini Afrika Kusini. Max Bushoke aliwahi kutamba sana nchini Tanzania alipokuwa na bendi kama vile Bima Lee Orchestra na nyinginezo. Vibao kama Mesenja Kaleta Balaa ni mojawapo ya vibao ambavyo Max hukumbukwa navyo sana.
Kwa upande wa Bushoke(Junior) kibao ambacho alitamba nacho sana na ambacho pengine ndio “kilichomtoa” rasmi ni kile kiitwacho Barua. Unaweza kukisikiliza kwa kubonyeza hapa.Kuna habari ambazo bado hatujaweza kuzithibitisha zinazosema kwamba Bushoke(Junior) naye ametimkia Afrika Kusini aliko baba yake ili kuendeleza shughuli zake za muziki.

No comments: