DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, August 29, 2013

Wyre: Naweza Tennis






Wyre The Love Child, Msanii wa muziki ambaye anafanya vizuri kutoka Kenya, ameweka wazi kuwa, mbali na kipaji kikubwa cha muziki alichonacho, yeye pia anapenda sana mchezo wa tenesi na ni mchezaji mzuri wa mchezo huo.

Wyre ambaye amefanikiwa kudumu katika muziki na kuendeleza mafanikio yake kwa muda sasa, amesema kuwa amekuwa akicheza mchezo huu na kuumudu sana, kitu ambacho watu wamekuwa hawakifahamu kumhusu.

Kwa sasa Wyre anaendeleza muziki wake ambao umefanikiwa sana kuvuka mipaka ya Afrika Mashariki, akiwa na rekodi yake inayofanya vizuri kwa sasa, inayokwenda kwa jina 'Nakupenda Pia' aliyofanya na Alaine kutoka Jamaica.

No comments: