DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Thursday, August 29, 2013

Young Dee agharamia Kideo




Baada ya kuachia video mpya ya ngoma yake ya “Kijukuu” ambayo imepokelewa poa na mashabiki wa muziki wake, Young Dee ambaye anafanya kazi zake za muziki chini ya lebo ya Authentic, ameongea na eNewz kuhusiana na kazi hii na video yake mpya ambayo ni ya tano kufanya tangu aanze muziki.

Young Dee ambaye hakutaka kuweka wazi gharama kamili za video hii, amesema kuwa kiukweli video hi imechukua kiasi cha pesa ambapo anakumbuka katika mchakato wa kutengenezwa kwake ilitokea pia tukio ambapo mtu mmoja kutoka timu yake aligonga gari la watu, tukio ambalo liliwalazimu kugharamia kulipa uharibifu miongoni mwa gharama nyingine za video.

Young Dee amesema kuwa katika video hii pia mtindo wa mavazi aliyotumia ni kutokana na uchauri wa rafiki zake pamoja na 'taste' ya Muongozaji video, ambapo ameweka wazi pia kuwa kiatu (buti) alilokuwa amevaa ni bidhaa ambayo imetengenezwa hapa hapa Tanzania... kitua ambacho wengi walikuwa hawafahamu.

No comments: