Fans wake hupendelea kumuita “King of Bongo Crunk”… jina halisi ni
Ilunga Khalifa a.k.a CPwaa! Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania
ambaye baada ya ukimya mrefu sasa kuachia kazi zake mpya.
C.P a.k.a CPwaa mwenye tuzo 3 za Tanzania Kilimanjaro Music Awards na
Multiple Channel O Africa Music Video Awards nominations anakuja
kivingine kabisa mwaka huu. Tarehe 1 mwezi wa October 2013, CPwaa
ataachia single yake mpya na ya kwanza kabisa kwa mwaka huu.Single hiyo
iitwayo “Chereko Chereko” yenye mahadhi ya AfroDance imefanywa chini ya
studio za ‘De Fatality Music” na producer “Mesen Selekta” ambaye mwaka
huu alichukua tuzo ya mtayarishaji bora Tanzania anayechipukia.Nyimbo
hii itapatikana kwenye mitandao yote na media zote kuanzia tarehe moja
October.
Kifuatacho baada
ya nyimbo hizi kutoka ni video zake ambapo Chereko Chereko itafanyiwa
Tanzania na Cross Border Therapy kufanyika nchini Afrika ya kusini. Kwa
wale mashabiki ambao watakuwa na kiu ya wimbo wa Cross Border Therapy
ambao utatoka mwakani wataweza kuupata wimbo huo kupitia iTunes,Amazon,
Spotify na digital store zingine bila kusahau mtandao wa “The Kleek” kwa
wale watumiaji wa smartphones za Samsung na Androids.
Asanteni sana na tuendelee kutoa support kwa wasanii wetu na muziki wetu.
No comments:
Post a Comment