DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Tuesday, September 24, 2013

Wasanii Wakubwa EAST AFRICA Kuungana Leo Kwenye EAST AFRICA WE ARE ONE – Radio Citizen Kenya @MzaziWillyTuva

Kenyan_flag 


Ni kupitia kwa show ya mtangazaji Mzazi Willy M. Tuva wa Citizen Radio, yaani WAKILISHA EA ambae leo atakuwa na show maalum kwa ajili ya wahanga wa tukio la kituo cha biashara cha WestGate …itakayofahamika kama  ‘East Africa We Are One’
Willy ata-dedicate show hiyo ambayo huwakutanisha wasanii wakubwa kutoka Afrika Mashariki akiwemo MwanaFA, AY, Hussein Machozi na wengineo na mashabiki wao ikiwemo kuzindua videos zao mpya katika maeneo ya Tribeka’s Beka Lounge (opposite Nation Centre) kila siku ya jumanne kuanzia saa 11 jioni.
‘East Africa We Are One’ itakuwa na msaniii wa gospel kutoka Uganda, Ambassada na Jua Cali amabo wameshatangaza kuwepo … watu wanaruhusiwa kufika na bendera za Kenya au zinazowakilisha Afrika Mashariki kuonesha umoja na kujiunga na wahanga wa tukio hilo.

No comments: