DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Saturday, September 28, 2013

Bamboo: Sigeuki nyuma


 

Rapa maarufu kutoka Kenya, Bamboo ama Simon Kimani kwa jina rasmi ambaye amekuwa katika vichwa vya habari mbalimbali baada ya kutangaza kumgeukia Mungu na kuacha muziki wa dunia, ametolea ufafanuzi wa hatua yake hii, na kusisitiza kuwa hajaamua kuokoka ili kujipatia umaarufu wala pesa, ila dhumuni lake kubwa ni kutangaza habari za Mungu.

Bamboo amejikuta akizua mitazamo tofauti kutoka kwa watu na hii ni hasa kutokana na kumbukumbu kuwa msanii huyu aliwahi kutangaza kuokoka tena kipindi cha nyuma, na baada ya muda akageuka tena na kurudia maisha ya kujichanganya.

Bamboo amesisitiza kuwa kwa sasa anajielewa zaidi na hatajali kile watu wanachofikiria ama kuendelea kusema juu yake.

No comments: