DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!
Friday, September 6, 2013
Davido anunua Gari bei mbaya
Muziki umeendelea kuwafaidisha wasanii na kuwasaidia kuishi katika ndoto zao, na hii imethibitika kwa mara nyingine hasa baada ya msanii Davido kutoka Nigeria, kuamua kufunga macho na kununua gari mpya yenye thamani ya dola 130,000 ambayo ni zaidi ya shilingi milioni 209 za Tanzania.
Gari hii mpya ya Davido ni Mercedes Benz G63AMG 2013 SUV, gari yenye hadhi na ya kifahari kabisa ambayo imevuta hisia za wengi mtandaoni kujadiliana juu ya uwezo wa kipesa wa msanii huyu na hatua ya kununua gari ya pesa nyingi namna hii.
Msanii huyu ndiye aliyeweka habari za kufanikisha mpango wake wa kununua gari hii kupitia twitter, ambapo aliweka picha ya gari hii na maneno yanayosomeka 'My baby fresh out the paint shop! Next Stop the port! See u in Lagos baby!!!".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment