DJ BOSTON-ON BEAT U KNOW WAT IT IS!!!

Friday, September 6, 2013

Bebe Cool, Goodlyf kuchuana

Lile tamasha maarufu ambalo huwa linawakutanisha na kuwapambanisha wakali wa muziki nchini Uganda, Battle Of The Champions limerudi tena kwa mwaka huu ambapo safari hii linatarajiwa kuwapambanisha Goodlyfe Crew pamoja na Bebe Cool. Tamasha hili ambalo ni mpambano mkali pia linatarajiwa kufanyika mwezi Desemba tarehe 6, na stori za chini ya zulia pia zinaweka wazi kuwa, Bebe Cool tayari amekwishadai shilingi milioni 200 za Uganda kwa ajili ya kuhakikisha ushiriki wake katika mpambano huu. Itakumbukwa kuwa mwaka jana pia Tamasha kama hili lilifanyika na kuwapambanisha Bebe Cool na hasimu wake wa muda mrefu, Bobi Wine ambao walionyesha uwezo wao jukwaani na mwisho wa siku umati wa mashabiki uliweza kuamua ni nani anaweza zaidi ya mwenzake.

No comments: